Achomwa moto mpaka kufa kisa debe tatu za mpunga
30 May 2024, 8:30 am
Matukio ya vijana kujihusisha na wizi yamekuwa yakitajwa kushamili hasa kwa maeneo ya vijijini wilayani Sengerema kutokana wananchi wengi kuvuna mazao ambapo chanzo chake kinadaiwa kuwa baadhi ya vijana kujihusisha na michezo ya kamali bila chanzo kingine cha kipato.
Na:Emmanuel Twimanye
Kijana mmoja ambaye hajafahamika jina lake amedaiwa kuuawa kwa kuchomwa moto na watu wasiojulikana kwa madai ya kuiba mpunga katika kitongoji cha Kanyele Kijiji cha Kang’hwashi Kata ya Nyamizeze Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza .
Wakizungumzia tukio hilo baadhi ya wananachi wamesikitishwa na tukio hilo na kuwaomba vijana kuachana na vitendo vya wizi.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kanyele Mathayo Kimoga Lyaloka amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo huku akiwataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi.
Naye mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Sengerema Mh,Senyi Ngaga ameitahadharisha jamii kuachana na tabia ya wizi badala yake wafanya kazi halali zitakazowasaidia kujipatia kipato.