CCM yamutwisha zingo la mradi wa maji Sengerema RC Mtanda
24 May 2024, 7:35 pm
Kamati ya Siasa mkoa wa Mwanza Ikiongozwa na mwenyekitiwa Chama cha mapinduzi (CCM) Michael Lushinge (SIMART) imekagua Miradi yenye thamani ya Tsh.Bil.20 ambapo ni pamoja na mradi wa Maji Nyasigu- Lubungo – Ngoma kata ya Igalula, Ujenzi wa daraja la Bugakara, Jengo la Utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, Ujenzi wa jengo la Mamlaka ya Mapato Wilaya ya Sengerema na Ujenzi wa uwanja wa Michezo Mnadani .
Na:Said Mahera
Chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Mwanza kimemtaka mkuu wa mkoa huo Said Mtanda kuhakikisha feha zilizobaki kwa ajili ya kukamilisha mradi wa maji uliyopo kijiji cha Nyasigu kata ya Igalula Wilayani Sengerema zinatolewa kwa wakati ili mradi huo uweze kukamilika kwa wakati.
Akitoa maagizo hayo mwenyekiti wa Ccm Mkoa wa Mwanza Ndg Michael Lushinge kwa niaba ya kamati ya siasa ya mkoa amesema kuwa imeridhishwa na hatua ya ujenzi wa maradi huo wa maji na kumuagiza mkuu wamkoa wa mwanza kuhakikisha fedha zilizobakia ziweze kutolewa ili kuweza kukamilika kwa mradi huo kwa wakati.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa mwanza Ndg Said Mtanda amemuahidi mwenyekiti wa ccm mkoa wa mwanza kutekeleza yale aliyoyaelekeza katika mradi huo.
Awali akisoma taarifa ya mradi huo Mkurugenzi mtendaji wa mamlaka wa maji safi na usafi wa mazingira Sengewrema (SEUWASA) Injini Sadala Hamisi amesema mradi huo utakapokamilika utahudumia Zaidi ya wakazi elfu hamsini.
Hata hivyo mkuu wa wilaya ya Sengerema Mh Senyi Ngaga amesema mradi huo ulianza kwa kukisuasua lakini kwasasa unaendelea vizuri.
Miradi iliyokaguliwa na kamati ya siasa mkoa wa mwanza ni pamoja na mradi wa maji nyasigu uliopo kata ya igalula ,ujenzi wa daraja la bugakara,jengo la halmashauri ya sengerema na ujenzi wa jengo la mamlaka ya mapato wilaya ya sengerema pamoja na uwanja wa michezo uliopo mnadani ikiwa miradi yote inagalimu kiasi cha bilioni 20.