Chama cha Mapinduzi cha shinda udiwani Kata ya Buzilasoga Sengerema
22 March 2024, 6:38 am
Kata ya Buzilasoga ni miongoni mwa kata 22 za Tanzania bara ambazo tume ya uchaguzi ilitangaza kufanyika uchaguzi mdogo katika kata hizo ambapo mgombea wa chama cha mapinduzi ndiye aliyetangazwa kuibuka mshindi kati ya wagombea wengine nane kutoka vyama tofauti.
Na:Emmanuuel Twimanye
Mgombea udiwani wa chama cha Mapinduzi (CCM) Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza Edina Godwin Bandihai ameshinda katika kinyang,anyiro cha uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata ya Buzilasoga kwa kupata kura 5227 .
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo Msimamizi wa uchaguzi katika Halmshauri ya Wilaya ya Sengerema Binuru Shekidele amemtangaza mgombea udiwani wa chama cha mapinduzi CCM Edina Godwin Bandihai kuwa mshindi wa kiti cha udiwani katika kata ya Buzilasoga huku akifuatiwa na mpinzani wake Mhoja Mathias Lubinza kutoka chama cha (ADC) aliyepata kura 242.
Mgombea udiwani aliyeshinda udiwani kwa tiketi ya chama cha mapinduzi Wilayani Sengerema Edina Godwin Bandihai amewashukuru wapiga kura kwa kumchagua huku akiahidi kuwaletea maendeleao.
Nao baadhi ya wananchi wa kata ya Buzilasoga wamesema kuwa wanamatumaini makubwa na diwani huyo aliyechaguliwa huku wakimwomba kukamilisha ujenzi wa shule shikizi ya msingi kilabela pamoja na kukarabati miundombinu ya barabara.
Ikumbukwe kuwa wagombea waliokuwa wakichuana kuwania Kinyanganyiro cha kiti cha udiwani katika uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata ya Buzilasoga walikuwa ni pamoja na Edina Godwini Bandihai (CCM) ambaye ameibuka mshindi ,Deus Kabilondo Nkwabi (NLD) ,Mhoja Mathias Lubinza (ADC) Ramadhan Omary Said (UPDP) ,Said Ramadhan Abudul (SAU) Rehema Hussein Kheri (AAFP) ,Anna Sulwa Zengo (CCK) na Msafiri Joseph Nyamwitanga (Demokrasia makini.