Wanusurika kifo baada ya kula samaki wanaodaiwa kuwa na sumu Sengerema
8 February 2024, 7:23 pm
Matukio ya watu kula samaki wanaodaiwa kuwa na sumu hutokea kwa baadhi ya maeneo hapa nchini ambapo katika kijiji cha Igaka ndio mara ya kwanza kutokea.
Na:Said Mahera
Watu saba wa familia moja wamenusulika kifo baada ya kula mbonga aina ya samaki inayosadikiwa kuwa na sumu katika kitongoji cha Igaka Senta Wilayani Sengerema mkoani Mwanza.
Wakisimulia tukio hilo baadhi ya wanafamilia walionusulika kufa baada ya kutumia samaki hiyo wamesema baada ya kula gafra wakaanza kuumwa tumbo na kupelekwa katika zahanati iliyopo kijijini hapo.
Naye baba wa familia iliyonusulika Ndg Edson Simba amesema baada ya kununua samaki yule na kumpeleka nyumbani kwa ajili ya maandalizi ya kutumika usiku, yeye alitoka na kuelekea sengerema,ndipo alipopigiwa simu na kupewa taarifa ya familia yake kuuguwa baada ya kula samaki huyo.
Kwa upande wao majirani akiwemo mchungaji wa kanisa la AICT igaka wamesikitishwa na tukio hilo huku wakilani tukio hilo la kushangaza huku mchungaji akiwaomba watu kuwa na hofu ya mungu.
Hata hivyo muhudumu wa afya ngazi ya jamii ndg Magambo Kengele amesema baada ya kuwapokea wagonjwa hao amewapa huduma ya kwanza kwa kuwanywesha maziwa na baadae kuwapeleka hospitalini kwa matibabu zaidi.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo mwenyekiti wa kitongoji cha igaka senta Bwn Emanuel Thobias amesema watu hao kutoka familia moja baada ya kula samaki matumbo yalianza kuuma na kukosa nguvu na kupelekwa katika hospitali.