37 wakutwa na kipindupindu Sengerema
1 February 2024, 3:12 pm
Licha ya Serikali kutoa vifaa tiba na kinga vyenye thamani zaidi ya Sh milioni 7 kwenye mikoa mitatu ya Kanda ya Ziwa kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu pamoja na dawa za kutibu maji kwa kuua wadudu wenye vimelea vya ugonjwa huo bado changamoto inazidi kuwa kubwa hasa maeneo ya kandokando ya ziwa victoria.
Na:Emmanuel Twimanye
Zaidi ya watu 37 wameripotiwa kuugua ugonjwa wa Kipindupindu Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza .
Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Mh,Senyi Nganga January 31 2024 ambapo amesema kuwa watu hao waliougua ugonjwa huo wamelazwa katika Kituo cha afya Katunguru ,Kituo cha Ngomamtimba na Hospitali teule ya wilaya ya Sengerema kwa ajili ya kupatiwa matibabu .
Kufuatia uwepo wa ugonjwa huo Wilayani humo Mkuu wa wilaya amewatahadharisha wananachi kuacha kusalimia kwa kushikana mikono pamoja na kuendelea kufanya usafi wa mazingira katika maeneo yao ili kukabiliana na ugonjwa huo.
Nao baadhi ya wananchi wilayani humo wameahidi kuchuakua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo.