Milioni 147 zatumika ukarabati wa madarasa shule ya msingi Sengerema
27 January 2024, 8:26 pm
Shule ya Msingi Sengerema ni miongoni mwa shule kongwe nchini ambayo ilikuwa ikikabiliwa na uchakavu wa miundombinu hasa vyumba vya madarasa jambo lililopelekea wadau mbalimbali kujitokeza na kuanza kusaidia ukarabati.
Na;Emmanuel Twimanye.
Shirika lisilisolikuwa la Kiserikali la Suport school Fees Foundation kutoka nchini Uholanzi limekarabati majengo 16 katika shule ya msingi Sengerema yenye thamani ya shilingi Milioni 147.
Akisoma taarifa ya ukarabati wa majengo hayo katibu wa shirika la Eco Faming Organisation Peter Mponeja linalofanya kazi kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ikiwemo shirika la Suport school Fees amesema kuwa wamefanikiwa kukarabati majengo 16 kati ya majengo 22 na kwamba majengo sita yaliyobaki yanatarajia kukarabatiwa muda sio mrefu.
Mkurugenzi wa shirika la Suport School Fees Slyvian Mshjuis amesema kuwa shirika hilo lililenga kuwasaidia kuwalipia ada wanafunzi shuleni lakini kwa sasa wamejikita kuwasaidia wanafunzi wengi zaidi .
Mkuu wa wilaya ya Sengerema aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo ya uzinduzi wa majengo hayo kwa Niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Amos Makala amelipongeza shirika hilo kwa kukarabati majengo hayo ili kuwasaidia wanafunzi kusoma katika mazingira rafiki.
Awali akisoma taarifa ya shule ,Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Sengerema Mwl,Samson Mafuru amesema kuwa baada ya ukarabati wa majengo hayo wanatarajia kuongezeka kwa mahudhurio ya wanafunzi kutoka asilimia 90 hadi asilimia 100 pamoja na kuongezeka kwa ufaulu wanafunzi katika mitihani ya ndani na taifa huku akilishukru shirika hilo kwa kuboresha shule hiyo.