DC Sengerema ageuka mbongo murundikano wa uchafu mjini
23 January 2024, 9:42 pm
Pamoja na kuwepo kwa taarifa za ugonjwa wa kipindupindu Nchini Madampo mjini Sengerema yanaonekana kujaa uchafu hali inayoleta wasiwasi kwa wananchi wakihofia kukumbwa na mlipuko wa ugonjwa huo.
Na;Emmanuel Twimanye.
Wafanyabishara wa soko kuu mjini Sengerema wameilalamikia Halmshauri ya Wilaya ya Sengerema kwa kuchelewa kuondoa taka zilizopo katika dampo la soko hilo , hali inayohatarsisha usalama wa afya zao katika kipindi hiki cha mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu.
Wametoa malalamiko hayo baada ya mkuu wa wilaya ya Sengerema Mh.Senyi Ngaga kutembelea na kukagua hali ya usafi katika soko hilo na kusema kuwa taka hizo zimedumu kwa muda mrefu bila kuondolewa na wahusika licha ya wafanyabishara kutoa tozo ya taka .
Mkurugenzi mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Sengerema Binuru Shekidele ameahidi kuondoa taka hizo kwa wakati ili kuwaondolea kadhia hiyo.
Naye Mkuu wa wilaya ya Sengerema Mh,Senyi Ngaga amemwagiza mkurugenzi mtendaji na afisa afya Wilbard Muyumbu kuhakikisha wanaondoa taka hizo kila siku na si vinginevyo.