Sengerema FM

Watu wanne waangukiwa na ukuta wa Nyumba

17 January 2024, 5:35 pm

Picha ya nje ya muonekano wa Hospitali teule wilaya ya Sengerema Mission walipo lazwa majeruhi hao. Picha Emmanuel Twimanye.

Kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha baadhi ya maeneo nchini zimesababisha nyumba nyingi kuanguka huku nyingine zikiwa katika hali tete ya nyufa, ambapo viongozi wengi wamekuwa wakitoa tahadhali kwa wananchi kuhama kwenye maeneo yenye changamoto au mkondo wa maji.

Na:Emmanuel Twimanye

Watu wanne wa Familia moja  wameangukiwa ukuta wa nyumba na kujeruhiwa sehemu mbalimbali za miili yao katika Kijiji cha Ngoma Kata ya Igalula Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza .

Wakizungumzia tukio hilo  wakiwa wamelazwa katika Hospitali teule ya Wilaya ya Sengerema (SDDH)  baadhi ya wathirika wamesema kuwa  baada ya kuangukiwa na ukuta waliokolewa na wasamalia wema na  kupelekwa  katika kituo cha Afya Kagunga kisha  kupewa rufaa ya kwenda Hospitali teule ya wilaya ya Sengerema kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Nao baadhi ya ndugu  wamesikitishwa na tukio hilo na  kuiomba jami kuwa makini katika kipindi hiki cha mvua. 

Kufuatia tukio hilo Mwenyekiti wa Kijiji cha Ngoma Bwn. Subi Mkonole na Afisa mtendaji wa kata ya Igalula Jenipha Mashamba wamewatahadharisha wananchi kuwa makini dhidi ya mvua zinazoendelea kunyesha ikiwa ni pamoja na kuhama kwenye nyumba  zilizochoka ili kunusuru maisha yao.

Taarifa ya Mwandishi wetu Emmanuel Twimanye inafafanua zaidi.