RC Mwanza aipongeza Sengerema ujenzi wa madarasa.
16 January 2024, 4:48 pm
Mkuu wa mkoa wa mwanza Mh, Amos Mkala baada ya kutamatisha ziara yake katika Halmshauri ya Sengerema, ameendelea na ziara yake katika Halmshauri ya Buchosa wilayani Sengerema kwa ajili ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo sekta ya elimu.
Na: Jovina George.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh, Amos Makala amewapongeza viongozi wa chama na Serikali Wilayani Sengerema kwa kujenga madarasa katika shule ya msingi Pambalu.
Mh, Makala ametoa pongezi hizo baada ya kutembelea katika shule hiyo na kukagua miundombinu ya vyumba vya madarasa na kukuta zoezi la ujenzi linaendelea vizuri, huku akiunga mkono ujenzi huo kwa kutoa shilingi milioni tano.
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) Wilayani Sengerema Mark Augustine Mkaoye amesema kuwa shule hiyo inawanafunzi wengi hivyo bado inahitaji vyumba vya madarasa ili kukidhi mahitaji ya wanafunzi .
Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Sengerema Mh,Yanga Makaga amemhakikishia mkuu wa mkoa kuwa fedha zilizobaki kati ya milioni sabini zitakamilishwa na Halmshauri na kuanza ujenzi mara moja .
Awali akitoa taarifa ya shule kwa Mkuu wa Mkoa ,Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Pambalu Mwl. Sundi Mussa amesema kuwa shule hiyo inakabiliwa na upungufu wa madarasa 24 , madawati 183 na matundu 56 ya vyoo pamoja na ukosefu wa nyumba za walimu.