Wananchi watakiwa kuchukua tahadhali ya kipindupindu
10 January 2024, 6:25 pm
Changamoto ya kipindupindu imetajwa kuenea kwa kasi zaidi hasa kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa ikianzia katika wilaya ya Bariadi mkoa wa Simiyu, ambapo mpaka sasa katika mkoa wa Mwanza wamebainika wagonjwa wa kipindupindu 27 kwenye maeneo ya wilaya ya Magu na Mwanza jiji.
Na:Emmanuel Twimanye.
Wananachi Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza wametahadharishwa kujikinga dhidi ya ugonjwa wa Kipindupindu hususani katika kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha.
Tahadhari hiyo imetolewa na mtaalamu kutoka ofisi ya Mganga mkuu wa Halmshauri ya Wilaya ya Sengerema Charles Manyanga kufuatia ugonjwa huo kutokea katika Halamshauri ya Nyamagana na Ilemela Mkoani Mwanza.
Katika hatua nyingine mtaalamu huyo ameitaka jamii kutoficha taarifa za wagonjwa badala yake watoe taarifa kwa afisa mtendaji wa kijiji ama wa kata ili wagonjwa wapelekwe haraka kwenye kituo cha kutolea huduma kwa ajili ya kupatiwa tiba stahiki.
Nao baadhi ya wananchi wilayani humo wameahidi kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo .