Taka zazua taharuki kwa wakazi wa Mission Sengerema
25 October 2023, 6:54 pm
Kwa muda mrefu sasa Halmashauri ya Sengerema imekuwa ikikabiliwa na changamoto la murundikano wa taka kwenye vizimba vya taka vilivyopo maeneo mbalimbali mjini, jambo hili limepelekea baadhi ya wafanya usafi kuzoa kwenye vizimba na kwenda kuzitelekeza kwenye makazi ya waatu eneo la Mission na kuleta taharuki kwa wakazi wa eneo hilo wakihofia kukumbwa na magongwa ya mulipuko.
Na:Emmanuel Twimanye.
Wakazi wa Kitongoji cha Misheni Wilayani Sengerema wamelalamikia kitendo cha wafanya usafi kugeuza makazi yao kuwa dampo la taka kwa kipindi cha zaidi ya miaka 2 hali inayohatarisha usalama wa afya zao hususani katika msimu huu wa mvua.
Wakizungumza na Radio Sengerema wamesema kuwa wafanya usafi hao hubeba taka kisha kwenda kumwaga karibu na makazi yao na kusababisha mlundikano wa taka huku wakihofia kukumbwa na magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu.
Wafanya usafi katika kata hiyo wamesema kuwa wanafanya hivyo kutokana na kukosa eneo maalumu la kuhifadhia taka huku wakiutuhumu uongozi wa kitongoji hicho kuwaelekeza kumwaga taka karibu na makazi ya watu.
Mwenyekiti wa kitongoji cha misheni Joseph Protas amekanusha madai hayo na kusema kuwa amekwisha piga maruku wafanya usafi kumwaga taka katika eneo hilo na kwamba hayo ni maamuzi waliyojichukulia wafanya usafi na si vinginevyo .
Kufuatia hali hiyo Mkurugenzi mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Sengerema Binuru Shekidele ameahidi kufika katika eneo hilo ili kushughulikia suala hilo haraka iwezekanavyo.