UWT yawataka wazazi kutoa malezi bora kwa watoto wenye mahitaji maalumu
24 October 2023, 2:48 pm
Shule ya Msingi Sengerema kitengo maalumu ilianzishwa Rasmi mwaka 2003 ambapo mpaka sasa inauwezo wa kuhudumia watoto wenye mahitaji maalumu Zaidi ya 247, na bweni inaweza hudumia watoto 104 , Wazazi wanapaswa kuwapa nafasi watoto hao ya kupata haki yao ya Elimu kutoka na Serkali kuendelea kuimalisha miundo mbinu.
Na:Joyce Rollingstone.
Wazazi na walezi wilayani sengerema mkoani mwanza, wametakiwa kushirikiana na walimu wa shule ya Msingi Sengerema kitengo katika kuwalea watoto mwenye mahitaji maalumu.
Hayo yamebainishwa na mwenyekiti wa umoja wa akinamama wa (CCM, UWT) kata ya Nyampulukano Wilaya ya Sengerema BI Tatu Jamal Seleman, wakati wa maadhimisho ya wiki ya UWT walipo tembelea shule hiyo na kutoa misaada ya vitu mbalimbali zikiwemo sabuni.
Aidha ameendelea kutoa wito kwa wazazi kujenga mazingila rafiki na watoto, pindi watakapowaona katika mazingira ambayo si ya shule waweze kuwalejesha shuleni au kutoa taarifa kwa walimu.
Kwa upande wake Mwalimu mkuu msaidizi shule ya Msingi Sengerema kitengo cha elimu maalumu BI Theodora J.Muzawena, amewashukuru akinamama wa UWT kwa kutenga muda wao na kuona umuhimu wa kuazimisha siku hiyo kwa kuwatembelea watoto wenye mahitaji maalumu.