Mtoto afariki kwa kushambuliwa na Fisi
5 July 2023, 1:54 pm
Kutokana na kuongezeka kwa matukio ya Fisi kushambulia watu na mifungo wilayani sengerema, hali hiyo imezua hofu, huku baadhi yao wakishindwa kufanya shughuli za maendeleo
Na:Emmanuel Twimanye
Mtoto mwenye umri wa miaka 5 aliyeshambuliwa na Fisi na kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake katika Kitongoji cha chamigumo Kijiji cha Nyantakubwa Kata ya Kaungamile Wilayani Senggerema Mkoani Mwanza amefariki Dunia.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha chamigumo Elias Malika amethibitisha mtoto mathias Enock kufariki Dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando Jijini Mwanza.
Baadhi ya wananachi wa Kitongoji hicho licha ya kusikitishwa na tukio hilo wametumia msiba huo kuiomba serikali kukabiliana na fisi hao ili kunusuru maisha ya wakazi wa eneo hilo kwa kuwa kwa sasa wanaishi kwa hofu kubwa.