Serikali yaboresha huduma za afya Sengerema vijijini
5 July 2023, 11:51 am
Kufuatia baadhi ya watu katika jamiii kuamini imani za kishirikina na kuamini zaidi waganga wa jadi, serikali imeanza kuboresha huduma za afya nchini.
Na: Elisha Magege
Kufuatia kuwepo kwa maabara kwenye zahanati ya Mayuya iliyopo kata ya Tabaruka halmashauri ya Sengerema mkoani Mwanza wananchi wa eneo hilo wametakiwa kujitokeza kupata vipimo katika zahanati hiyo.
Wakizungumza na Sengerema Fm muuguzi wa zahanati hiyo wamesema kwa sasa huduma ya vipimo na kulazwa akina mama wajawazito inatolewa katika zahanati hiyo, hivyo waache kukaa na magonjwa au kwenda kwa waganga wa kienyeji na badala yake wafiki kupata vipimo vya kitaalam.
Nao baadhi ya wananchi kijijini hapo wameipongeza serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia kwa kuwapelekea maabalra, umeme na maji katika zahanati hiyo.
Mh. Sospiter Busumabhu diwani wa kata ya Tabaruka amesema ataendelea kushirikiana na mbunge wa jimbo la Sengerema katika kuleta maendelea kwa wananchi wa kata ya Tabaruka huku akiahidi zahanati ya Mayuya kuipandisha hadhi na kuwa kituo cha Afya.
Uwepo wa maabara katika Zahanati ya Mayuya umewasaidia wananachi wa kijiji hicho na vijiji jirani kuacha kutembea umbari mrefuu kutoka kijijini hapo hadi Mission Mjuini Sengerema kutafta huduma ya Vipimo ambapo kwa sasa zahanati hiyo inatoa huduma za vipimo na kulazwa hasa wamama wajawazito