Sengerema FM
Sengerema FM
15 October 2021, 9:44 am

Amefanya ziara hiyo ya kushtukiza jana kutokana na kusuasua kwa ujenzi wa hoteli hiyo.
Mhe. Masanja amemuelekeza Mwakilishi wa Mradi huo kutoka TANAPA, Jeremiah Machibya kumsimamishia mkataba mkandarasi huyo kama ameshindwa kumaliza kazi kwa muda unaotakiwa.
“Kama mkandarasi kazi imemshinda tengueni mkataba muweke anayeweza kuimaliza kazi hii kwa wakati” Mhe. Masanja amesisitiza.
Mradi huo wenye gharama ya shilingi Bilioni 11 unaosimamiwa na TANAPA ulianza mwezi Aprili 2020 na ulitarajiwa kukamilika mwezi Aprili, 2021 lakini mkandarasi ameongezewa muda hadi mwezi Machi, 2022 na gharama za ujenzi zilizotumika mpaka sasa ni Bilioni 4.1.