Mbunge Tabasam akutana na kuzungumza na Wafanyabiashara Sengerema.
29 May 2021, 6:39 pm
Mbunge wa jimbo la Sengerema Tabasam Hamis Mwagao amekutana na kufanya mazungumzo na wafanya biashara wa jimboni kwake kuhusiana na changamoto wanazokabiliana nazo.
Baada kikoa hicho Tabasam ameahidi kushirikiana na wafanya biashara hao kutatua kero zinazowakabiri, huku akiiomba serikali kumuondoa kazini mara moja manager wa TRA kutokana na kukosa sifa za kuendelea kuitumikia wilaya hiyo.
Akizungumza kwa niaba ya wafanya biashara hao Mwenyekiti wa wafanya biashara soko kuu mjini Sengerema Bwn.Samwel Meshack Budaga amesema kumekuwepo na changamoto ya kutokuhusishwa kwenye mamzi yanayofanywa na mamlaka na badala yake wamekuwa wakilazimishwa kutekeleza mambo bila kujali maslahi yao.
Kwa pande wake kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Sengerema Ally Salim Ally amesema changamoto zote zilizowasilishwa na wafanya biashara hao watazifanyia kwa kushirikiana na tasisi zinazohusika kama vile mamlaka ya mapato Tra,Tarura na Tanesco.
Mwenykiti wa Chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Sengerema Ndg. Mark Augostine Makoye amesema chama kipotayali kushauri pale kitakapo hitajika huku akisema ni vyema pia mamzi ya viongozi Wilayani hapo kukishirikisha chama ili kuboresha Zaidi maslahi ya wafanya biashara hao.
Mbunge Tabasam ameahidi kufanya vikao na wafanya biashara pamoja na wananchi wa jimboni kwake vya mara kwa mara ili kuongeza ufanisi na utendaji kazi wa kushungulikia kero na changamoto zinazowakabiri wananchi jimboni kwake.