TASAF yatoa onyo kali kwa watakao tumia fedha za wanufaika kinyume na utaratibu.
28 May 2021, 4:09 pm
Mpango wa kunusuru kaya masikini TASAF awamu ya tatu kipindi cha pili katika Halmashauri ya Buchosa Wilayani Sengerema imejipanga kuwachukulia hatua kali za kisheria kwa watakao bainika kutumia fedha za Tasaf kinyume na utaratibu.
Hayo yameelezwa na Bwn,Donard Mzilai kutoka TASAF makao makuu Taifa wakati akitoa mafunzo ya kuwajengea uelewa wawezeshaji wa mpango wa Tasaf katika ukumbi wa jengo la Hosptal ya Halmashauri ya Buchosa.
Bwn,Mzilai amesema Tasaf imebaini kuwepo kwa changamoto mbalimbali katika kipindi kilicho pita hivyo kusababisha walengwa kushindwa kunufaika na Tasaf
Katika hatua nyingine amesema Tasaf awamu ya tatu kipindi cha pili itaanza kutoa fedha kwa walengwa kwa njia ya kielekitloniki kwa lengo la kuhakikisha usalama wa fedha kwa wanufaika
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo kutoka kata mbalimbali na ngazi ya Halmashauri hiyo wameipongeza Tasaf kwa mafunzo hayo kwani yatasaidia wao kufanya kazi kwa weledi huku wakipongeza uwepo wa mfumo wa utoaji fedha kwa walengwa kwa njia ya kielekitroniki.
Kwa upande wake katibu tawala wilaya ya Sengerema kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Sengerema Dr,Emmanuel Kipole amewataka washiriki wa mafunzo hayo kwenda kufanya kazi kwa weledi ili kuondoa malalamiko kwa walengwa.
Tasaf inatarajia kuvifikia vijiji 15 ambavyo vilikuwa vimebaki katika Halmashauri hiyo ambapo itakuwa imevifikia vijiji vyote 82 vya Halshauri ya Buchosa
Taarifa zaidi na Katemi Lenatus……….