Mwauwasa yakabidhi mradi mkubwa wa maji mjini Sengerema.
21 May 2021, 4:47 pm
Mamlaka ya maji mjini mwanza (MWAUWASA) wamekabidhi mradi wa maji kwa mamlaka ya maji mjini Sengerema uliojengwa kwa kiasi cha zaidi billioni moja hadi kukamilika na unatarajia kunufaisha watu elfu kumi uliopo katika kata ya Nyampande Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza.
Akisoma taarifa ya mradi wa maji wa nyampande meneja miradi (MWAUWASA) Mhandisi Gogadi Mgwatu kwa mgeni rasmi ambaye alikuwa mkuu wa Wilaya Sengerema Dkt, Emmanuel Kipole wakati wa kukabidhi mradi huo kwa Mkurugenzi wa (SEUWASA),mhadisi Robert Lupoja amesema mradi huo ulitengewa bajeti ya Zaidi ya Shilingi billioni moja mwaka 2017 baada ya agizo la aliyekuwa Rais wa awamu ya 5 hayati Dkt. Magufuli wakati wa uzinduzi wa mradi mkubwa wa maji wa Nyamazugo.
Kwaupande wake mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya maji mjini Sengerema(SEUWASA) amesaini na kupokea mradi huo na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano wao katika kulinda miundo mbinu ya maji ikiwa nipamoja na kutoa taarifa juu ya upasukaji wa mabomba ya maji.
Sambamba na hayo ,Diwani wa kata hiyo ya Nyampande Mh, George Kazungu John ameishukuru serikali kwa ujenzi wa mradi wa maji katika kata yake na kudhibitisha kuwa hadi sasa wananchi wake wananufaika na mradi huo wa maji.
Taarifa zaidi sikiriza hapo……