Naibu waziri Tamisemi atoa maagizo mazito kwa viongozi Sengerema.
10 May 2021, 4:20 pm
Naibu waziri wa Tamisemi Mh, David Erenest Silinde ameiagiza halmashauri ya Sengerema kulipa fidia kwa wananchi walioachia viwanja vyao kwa ajiri ya kupisha ujenzi wa stendi mpya ya magari eneo la bukala kata ya ibisabageni wilayani Sengerema Mkoani Mwanza ndani ya miezi minne.
Mh, Silinde ametoa agizo hilo kwa Kaimu mkururugezi halmashauri ya Sengerema bw, Ally Salimu wakati wa ziara yake yakikazi na kumtaka kushirikiana na madiwani kuhakikisha wanakusanya mapata ipasavyo ili kulipa deni la Zaidi ya million 84 ikiwa ni fidia ya wananchi walio achia viwanjwa kwa ajiri ya ujenzi wa stendi mpya ya magari katika eneo la bukara kabla ya tarehe tisa mwezi wa tisa mwaka huu.
Naibu waziri huyo amesikitishwa na hali hiyo ikiwa tangu wananchi hao wazuiliwe kufanya shughuli yoyote katika viwanja vyao ili kupisha ujenzi huo ikiwa hadi sasa ni takiribani miaka kumi bila kulipwa fidia.
Aidha, naibu waziri Slinde katika ziara yake ametembelea soko kuu mjini Sengerema,soko la Samaki la Migombani Pamoja na gulio la mnadani,sambamba na hayo ameweka jiwe la msingi katika ujenzi wa shule ya sekondari ya kata Nyampulukano, ujenzi wa shule ya sekondari katika kata ya ibondo na ujenzi wa shule ya sekondari kata ya ngoma halmashauri ya sengerema Mkoani Mwanza.
Taarifa zaidi na Amina Hassani……………………