Sengerema FM

TBS yatakiwa kufanya ukaguzi wa Bidhaa feki Mjini Sengerema.

5 May 2021, 5:05 pm

Manager mafunzo wa TBS akizungumza na washiriki wa mafunzo kwa katibu tawala wa (W) Sengerema

Shirirka la viwango nchina Tanzania TBS limetoa mafunzo ya usindikaji bidha za mchele kwa wajasilia mali Wilayani Sengerema mkoani Mwanza.

Akizungumza baada ya kufungua mafunzo hayo Katibu Tawala wa wilaya hiyo kwa niaba ya mkuu wa wilaya  Bwn. Alan augostine Mhina amewataka TBS kufanya ukaguzi wa bidhaa zinazozalishwa na kuingizwa wilayani Sengerema kwani kumekuwepo na baadhi ya wafanya biashara wanaouza bidhaa zisizo na ubora.

Sauti ya katibu tawala (W) Sengerema Bwn, Allani A.Muhina

Kwa upande wake meneja wa mafunzo na utafiti (RTMM) Mwl.Hamis  Sudi Mwanasala kwa niaba ya mkurungenzi mkuu wa shirika la viwango Tanzania TBS, amesema jambo hilo watalifanyia kazi la kuongeza wataalamu watakao kuwa wakifanya ukaguzi wa mara kwa mara wilayani hapo.

Sauti ya manager mafunzo TBS Mwl. Hamis S.Mwanasala

Naye Manager wa TBS Kanda ya ziwa Bwn,Ismail Joseph Mwaipaja amesema wameanda mafunzo haya maalumu kwa wajasiliamali wa bidhaa za mchele ili kuwawezesha namna ya kusindika na kufungasha bidhaa hizo.

Sauti ya manager wa TBS Kanda ya ziwa Bwn,Ismail J.Mwaipaja

Shirika la viwango Tanzania limeanza kutoa mafunzo ya ujasilia mali na usindikaji wa bidhaa za mchele kwa kushirikiana na mamlaka zingine kama SIDO pamoja na ofisi za halmashauri husika.