Sengerema FM

Rais Mama Samia kuhutubia wabunge rasimi, Ndugai atoa neno.

April 21, 2021, 6:28 pm

Sipika wa Bunge Job Ndugai akizungumza bungeni Dodoma

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai ameagiza mawaziri, manaibu mawaziri na wabunge, kurudi bungeni mara moja ili kuhudhuria hotuba ya Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan hapo kesho.

Spika ametoa maagizo hayo mapema leo Aprili 21, 2021, bungeni kwenye mkutano wa tatu kikao cha kumi na nne, ambapo amesema watachukua mahudhurio kwa kuwa kila mtu anatakiwa kuwa ndani ya Bunge wakati Rais anazungumza na taifa.

Sauti ya Sipika wa bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai

Katika kipindi cha maswali na majibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Mwigulu Nchemba amesema serikali inaibadilisha sekta ya kilimo kutoka kuwa ya kubahatisha kwenda kwenye sekta ya uhakika kwa kuwa sekta hiyo kwa sasa imekuwa ikiongoza kuwa na mikopo chechefu.

Swali la Halima mdee na majibu ya Waziri wa fedha na mpango. Dr. Mwigulu Nchemba