Sengerema FM

Mwadui FC yatamba kuvuruga mipango ya mabingwa wa ligi kuu Vpl Simba sc.

17 April 2021, 3:43 pm

Kocha wa mwadui fc Salhina Mjengwa akizungumzia metch yake dhiidi ya Simba sc, kulia kaptain wa klabu hiyo Mussa Mbisa

Kocha wa Mwadui Fc Salhina Mjengwa amesema amejipanga vilivyo kuikabilia klabu ya Simba sc kutoka jijini Dar es salaam katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara utakao chezwa siku ya jumapili ya tar18/04 mwaka huu katika uwanja wa Ccm kambarage mjini Shinyanga.

Akizungumza na wandishi wa habari kocha mjengwa amesema wapo tayali kufa na kupona kutetea pointi tatu mhimu kwa mnyama samba sc kwani kikosi chake kipo kamili hakuna majeruhi kwa mjibu wa daktari wa klabu hiyo yenye masikani yake eneo la Mwadui mkoani hapo.

Sauti ya Kocha wa Mwadui Fc Slhina Mjengwa.

Kwa upande wake Captain wa team hiyo Mussa Mbisa amesema wachezaji wezake wamejipanga kucheza mchezo mzuri huku akiwataka mashabiki wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi kuisuprt team yao.

Sauti ya Captain wa Mwadui Fc Mussa Mbisa

Naye mratibu wa Simba sc Bwn, Abas Ally amesema team hiyo imejipanga vikali kuwakabili Mwadui licha ya kuwa rekodi ya kupoteza katika uwanja huo lakina awamu hii amesema hawataki kupoteza tena.

Sauti ya mratibu wa Simba sc Said Ally

Shirikisho la mpira wa miguu mkoa wa Shinyanga limetangaza vingilio katika metchi hiyo ambapo kwa  VIP itakuwa ni Shilingi 10000 na kawaida ni Shilingi  elfu Tano na kwamba wameimalisha ulinzi katika uwanja kwa mashabiki na wachezaji