Zaidi ya bil.15 zatumika nje ya bajeti,CAG azianika tasisi zilizofanya hivyo.
8 April 2021, 2:00 pm
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere ameisoma ripoti yake ya mwaka wa fedha 2020/21 mbele ya waandishi wa habari leo Aprili 8, 2021 jijini Dodoma na kubainisha baadhi ya taasisi zikiwemo wizara zilizofanya manunuzi nje ya utaratibu.
CAG Kichere amesema ununuzi uliofanyika nje ya mpango wa mwaka wa manunuzi, umefanywa na jumla ya taasisi 7 ambazo ni TRA, Wizara ya Afya, Zimamoto, Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Manispaa ya Morogoro, Wizara ya mambo ya Nje, Wizara ya Mifugo na Uvuvi zilifanya ununuzi wa vifaa na huduma wa zaidi ya shilingi Bil 15.129.
Mbali na ripoti katika eneo hilo la manunuzi, CAG pia amezitaja Halmashauri, Manispaa pamoja na Taasisi ambazo zimepewa hati mbaya ikiwa ni pamoja na Halmashauri za Wilaya Shinyanga, Singida, Itigi na Igunga, Wilaya ya Sikonge, Urambo, Momba, Manispaa ya Tabora, Hospitali ya Rufaa Morogoro na Tume ya UNESCO
Ikumbukwe kuwa Machi 28,mwaka huu CAG Charles Kichere aliisoma ripoti hiyo na kuiwasilisha kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.