Sengerema FM

Zao la alizeti latajwa kunyanyua uchumi wa wananchi Sengerema

6 April 2021, 6:14 pm

Mmoja wa wakulima akipokea maelekezo kuhusiana na ulimaji bora wa zao la Alizeti

Afisa kilimo kata ya Nyatukala Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza  Bi. Jonesia Joseph amewataka wakazi wa kata hiyo kutumia mvua zinazoendelea kunyesha  katika  kilimo ili kujipati chakula  pamoja na kipato.

Bi Jonesia ametoa kauli hiyo ofisini kwake nakusema kuwa  kutokana na aridhi kuwa na kiasi kikubwa cha maji kwasasa hivyo wakulima wanapaswa kulima mazao ya muda mfupi kama vile viazi na mtama ili kuondokana na upungufu wachakula.

Aidha afisa kilimo huyo amewaasa wakulima kutumia maafisa ugani walioko katika kila semu katani humo ili kupewac elimu jinsi ya kujihusisha  na kilimo cha  alizeti ambacho ni cha mkakati kwa lengo la kujipatia kipato kupitia zao hilo.

Kata ya Nyatukala hujihusisha zaidi na kilimo cha  mazao ya chakula kama mahindi,nyanya na viazi hivyo ni vyema pia wakulima  kujihusisha na zao la alizeti ili kupata maligafi kwaajili ya viwanda ili  kujikwamua kiuchumi.