Sengerema FM

Mwalimu mstaafu awataka vijana kuiga mfano wa Hayati Dkt. Magufuli.

4 April 2021, 12:13 pm

Mwl. Solomon Elifuraha mwalimu aliyefundisha na hayati Dr. Magufuli somo la hisabati Sengerema Sekondari

Mzee Solomoni Elifuraha ni mwalimu mstaafu ambaye kafanya kazi na Hayati Dr. John Pombe Magufuli katika shule ya Senkondari Sengerema iliyopo mjini Sengerema Mkoani Mwanza.

Akizungumza kwa masikitiko makubwa Mwl. Elifuraha amesema alizipokea kwa mashituko makubwa taarifa za kifo cha Dr. Magufuli kwani hakuwa na taarifa yoyote ya ugonjwa wake.

Katika hatua nyingine amesema enzi za uhai wake kipindi baado ni mwali katika Shule ya Sekondari Sengerema Dr. Magufuli alikuwa muandilifu na mchapa kazi na pia alikuwa na ushirikiano na walimu wenzake shuleni pale.

Mwl. Elifuraha amesema Magufuli licha ya kuwakuta wakiwa kazini lakini yeye alifika na kununua kiwanja na kuanza ujenzi ambapo ndani ya miaka yake miwili alikuwa akiishi kwenye nyumba yake siyo kwenye Nyumba za Serikali.

Zaidi msikirize hapa Mwl. elifuraha akimzungumzia hayati Magufuli ……………