Sengerema FM

Issa Mustapha atumia pikipiki kutoka Dar hadi Chato kumzika JPM.

28 March 2021, 2:40 pm

Issa Mustapha akiwa katika kituo cha bodaboda mjini Sengerema

Mwananchi mmoja anayejulikana kwa jina Issa Mustapha amesafiri umbali wa zaidi ya kilomita 1,200,kutoka mkoani Dar es Salaam hadi wilayani Chato Mkoa wa Geita kwa kutumia bodaboda  kushiriki mazishi ya Hayati John Pombe Magufuli.

Akizungumza wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza akiwa njiani kuekea Dar es Salaam,  Mustapha amesema alichukua uamuzi huo kuenzi mchango wa Magufuli kwa madereva wa bodaboda kwa kuwa katika uongozi wake, walifanya kazi bila kusumbuliwa, nakwamba alishiriki shughuli ya kumuaga kiongozi huyo mkoani Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza na Wilaya ya Chato.

Mmoja kati ya madereva bodaboda mjini Sengerema amesema uamuzi wa mwenzao kusafiri umbali mrefu ili kumuaga Magufuli ni kitendo cha kiungwana na kinapaswa kuungwa mkono.

Hayati Dr.Magufuli alifariki dunia Machi 17, 2021 kwa ugonjwa wa moyo na mazishi yake yalifanyika katika kijiji cha Mlimani wilayani Chato Machi 26, 2021.