Pambazuko FM Radio

Ujenzi wa  zahanati kukamilika hivi karibuni

21 February 2023, 3:40 pm

Na Elias Maganga

Mwenyekiti wa Kijiji cha Machipi Halmashauri ya Mji wa Ifakara Wilayani Kilombero Bwana Philip Mwitumba amesema Ujenzi wa jengo la zahanati umefikia hatua ya kupaua na unatarajiwa kukamilika machi 16 mwaka huu.

Bwana Mwitumba amesema mradi wa ujenzi huo wa zahanati ulianza tangu mwaka 2021,mpaka sasa wananchi wamechangia nguvu kazi milioni 26 huku serikali ikiwachangia milioni 65.

Bwana Mwitumba amesema serikali itaendelea kutoa fedha kwa ajili ya umaliziaji kwa kila hatua ya ujenzi

Mwenyekiti wa Kijiji cha Machipi Halmashauri ya Mji wa Ifakara Wilayani Kilombero Bwana Philip Mwitumba {Picha na Elias Maganga}
Sauti ya Mwenyekiti Mwitumba akielezea ujenzi huo

 Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa zahanati hiyo Bwana Anania Mkumbwa amesema mpaka hapo ujenzi ulipofikia wamekumbana na changamoto kwa baadhi ya wananchi kuwa wazito kwenye uchangiaji wa shughuli za maendeleo

Bwana Mkumbwa amesema,a jengo hilo la zahanati litakamilika machi 16 mwaka huu na litazinduliwa na mbio za mwenge wa uhuru mei 5 mwaka huu na baada ya hapo litaanza kazi rasmi ya kuhudumia wagonjwa.

Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa zahanati hiyo Bwana Anania Mkumbwa{Picha na Elias Maganga}
Sauti ya Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa zahanati hiyo Bwana Anania Mkumbwa akielezea changamoto alizokutana nazo katika ujenzi hu unaoendelea

 Hamida Luambano ni Mjumbe msismamizi wa ujenzi huo anasema kukamilia kwa zahanati hiyo itawasaidia kwa kiasi kikubwa kuzogezewa huduma za afya kwani wamekua wakitembea umbali mrefu kufuata huduma za afya Kata ya Kibaoni

Hamida Luambano mkazi wa Kijiji cha nakatimbu{Picha na Elias maganga
Sauti ya Hamida akishukuru serikali kuwaunga mkono