Orkonerei FM

Kilio cha Akina Mama Oldonyo: Walazimika Kubebwa Mikononi Kuvushwa Korongoni Kufuata Huduma za Afya

17 March 2026, 9:51 am

Na Evanda Barnaba

picha na Evanda Barnaba

Wananchi wa Kijiji cha Oldonyo, Kata ya Lemooti wilayani Monduli wamelalamikia hali mbaya ya korongo linalowaunganisha na Kijiji cha Lolkisale wakisema limekuwa hatari na kusababisha kukosekana kwa huduma muhimu hasa kipindi cha mvua.

Agnes Gavana, mkazi wa Kijiji cha Oldonyo, amesema walilazimika kubeba mgonjwa kwa shida ili kuvuka korongo hilo baada ya kushindwa kupata usafiri.

Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Oldonyo, Saitoti Mwatumi, amesema serikali ya kijiji imejaribu kufanya marekebisho ya muda lakini ardhi ya eneo hilo ina mmomonyoko mkubwa. Amesema tayari viongozi wa eneo hilo wamewasilisha taarifa kwa mamlaka husika ili kupata suluhisho la kudumu kama ujenzi wa daraja au kalvati katika korongo hilo.