Orkonerei FM
Orkonerei FM
17 February 2026, 2:16 pm

Picha kwa msaada wa mtandao
Serikali na wadau wa afya nchini wameendelea kusisitiza umuhimu wa mama wajawazito kujifungulia katika vituo vya afya na zahanati ili kuhakikisha usalama wa mama na mtoto.
Na Baraka David Ole Maika
Pamoja na juhudi za serikali na wadau wa afya kusisitiza umuhimu wa mama wajawazito kujifungulia katika vituo vya afya na zahanati, baadhi ya jamii bado zina imani potofu na kuendelea kutumia wakunga wa jadi kujifungulia nyumbani, jambo ambalo limekuwa likitajwa kuchangia vifo vinavyoweza kuepukika kutokana na ukosefu wa vifaa na utaalamu wa dharura.
Katika kijiji cha Terrat Simanjiro, baadhi ya familia wameanza kubadili mwelekeo huo, wakiongozwa na familia ya Elrehema Jonas ambao wameshirikisha uzoefu wao kuhusu tofauti ya uzazi wa sasa na wa zamani na kueleza jinsi maandalizi ya mapema na uangalizi wa madaktari unavyoweza kuokoa maisha,
MWANDISHI WETU BARAKA OLEMAIKA AMETEMBELEA FAMILIA HII NA KUTUANDALIA TAARIFA HII