Orkonerei FM
Orkonerei FM
3 February 2026, 11:49 am

Na Dorcas Charles
Wakati CCM ikiazimisha miaka 49 tangu kuasisiwa kwake mwaka 1977, Katibu wa CCM Wilaya ya Simanjiro, Bi. Wambura Igembya, ameelezea mabadiliko makubwa ya kijamii na kiuchumi yaliyopatikana wilayani humo.
Katibu amebainisha kuwa tangu kuzaliwa kwa chama hicho, kumekuwa na maboresho ya dhahiri katika sekta za afya, hususan afya ya mama na mtoto, ujenzi wa miundombinu ya shule, na barabara.
Akizungumzia na na mwandishi wetu Dorcas Charles Bi. Igembya amesema kuwa changamoto za ardhi ambazo zimekuwa zikiwakabili wakulima na wafugaji, Katibu Igembia amesisitiza kuwa Ilani ya CCM imetoa mwelekeo madhubuti wa kutatua migogoro hiyo.
Alibainisha kuwa tayari Mwenyekiti wa CCM Mkoa, Ndg. Peter Toima, ametoa maelekezo kwa makatibu na viongozi wa chama kuhakikisha migogoro ya ardhi inashughulikiwa kwa haki na weledi.
Karibu kusikiliza mahojiano hayaa.