Orkonerei FM
Orkonerei FM
30 January 2026, 11:18 am

Na Nyangusi Olesang’ida
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Laizer, kata ya Oligilai Mkoani Arusha Willguard Eliakimu Medukenya, amewataka wananchi wa Kata ya Oligilai kujitokeza kujiandikisha kwa Diwani wa Kata ili kupata huduma ya umeme kupitia mradi wa REA. Mwedukenya ametoa wito wa ushirikiano miongoni mwa wakazi hao na kuwaonya kutokubali kupotoshwa na itikadi za kisiasa, akisisitiza kuwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii yatafikiwa tu iwapo wananchi wataungana na kulinda kitongoji chao.
Mwenyeikiti Huyo ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye kipindi cha Amsha Amsha na Nyangusi Olesang’ida
katika hatua nyingine Mwenyekiti Medukenya, amebainisha kuwa uongozi wake umefanikiwa kurejesha haki za wananchi kwa asilimia 100, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha fursa za serikali zinawafikia walengo. Akizungumzia mafanikio hayo, Mwedukenya amesema wamefanikiwa kugawa viwanja katika eneo la Meru Forest kwa ajili ya wajane na watu wasiojiweza, huku wakihakikisha barabara zote za ndani zinapitika na kulinda mipaka ya maeneo ya umma dhidi ya uvamizi.