Orkonerei FM

Makala ya kurunzi kuhusu matumizi ya AI

7 November 2025, 10:16 am

Simu ikiwa katika ukurasa wa Akili Unde (AI). Picha kwa msaada wa mtandao

Kutokana na uwezo wake wa kuboresha huduma katika sekta mbalimbali kama vile afya, elimu, usafiri, na biashara, AI inatoa faida nyingi

Na Dorcus Charles

Katika ulimwengu wa leo, teknolojia ya Akili Bandia (AI) imekuwa sehemu muhimu ya maisha yetu ya kila siku. Ingawa wengi wanaitumia, si wengi wanajua jinsi gani wanavyoweza kulindwa na faida na changamoto zinazohusiana na matumizi ya AI. Kutokana na uwezo wake wa kuboresha huduma katika sekta mbalimbali kama vile afya, elimu, usafiri, na biashara, AI inatoa faida nyingi.

Kwenye kipindi cha Kurunzi Maalum kinachorushwa kila Ijumaa saa mbili na nusu asubuhi hapa Orkonerei FM, mwandishi Dorcas Charles amezungumza na wataalamu mbalimbali na wananchi kuhusu jinsi AI inavyobadilisha maisha yao.