Orkonerei FM

‘Chanjo ya mbwa ni kinga ya maisha’

3 October 2025, 1:30 pm

Kurunzi Maalum

Katika jitihada za kukabiliana na ugonjwa hatari wa kichaa cha mbwa, jamii na serikali zinahimizwa kushirikiana ili kuhakikisha idadi kubwa ya mbwa wanapata chanjo kila mwaka. Ugonjwa huu, unaosababishwa na virusi, bado unaendelea kuwa tishio kwa binadamu na wanyama wengine, hasa katika maeneo ya vijijini.

Kwa mujibu wa utafiti, mbwa 164,000 walipimwa na 86,000 walichanjwa, sawa na takriban asilimia 52 ya mbwa wote. Hii inaonyesha bado kuna pengo kubwa, kwani karibia asilimia 48 ya mbwa hawajafikiwa na chanjo muhimu.

Katika kipindi maalum cha “Kurunzi” kinachorushwa na Orkonerei FM Radio, mwandishi Dorcas Charles amechambua umuhimu wa chanjo kwa mbwa na paka. Mada hii ilihusisha ushuhuda wa mkaazi wa Terrat, Bwana Pendaeli John, ambaye aliwahi kung’atwa na mbwa mwenye kichaa.

Unaweza kusikiliza kipindi kizima cha “Kurunzi” ili kupata maelezo zaidi juu ya mada hii muhimu.