Orkonerei FM
Orkonerei FM
1 October 2025, 6:22 pm

Picha Na Joyce Elias
Wazazi wa watoto wanaosoma katika shule ya msingi terrat wilaya ya simanjiro wamehimizwa kushirikiana na uongozi wa shule kuboresha huduma za chakula kwa wanafunzi.
Akizungumza Katika kikao cha wazazi na uongozi wa shule hiyo Mwenyekiti wa kamati ya shule Bwana Israel Mesiyaki Mollel amesema kuwa wazazi wanatakiwa kufuata masharti waliojiwekea ili kutowapa kazi ya ziada waalimu.
Akizungumza na Mwandishi wa Orkonerei Radio Joycye Elius Mwalimu mkuu wa shule hiyo Deo Lusian Osoki amesema kuwa lengo la kikao hicho ni kuiboresha taaluma na kwamba wazazi na walimu wanashirikiana vizuri ili kufatilia maendeleo ya watoto yao.