Orkonerei FM
Orkonerei FM
17 May 2025, 12:00 pm

Nijuze Radio Show
Katika toleo hili maalum la Nijuze Radio Show, Dorcas Charles na Isack Dickson wanatembelea kata ya Endiamtu, ndani ya Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mirerani Simanjiro mji wa Tanzanite, ndoto, vijana na harakati. Kipindi kinachunguza kwa undani hali ya afya ya uzazi kwa vijana, upatikanaji wa huduma, changamoto, mitazamo, na uhalisia wa maisha ya vijana wa Mirerani.
Kutoka kwenye ofisi ya kata, vijiweni, barabarani, kwenye maduka ya dawa hadi Kituo cha Afya Mirerani, timu ya Nijuze inakusanya simulizi halisi:
– Vijana wanaeleza ugumu wa kupata huduma za afya ya uzazi
– Wazazi na viongozi wanatoa maoni yao
– Na Afisa Muuguzi Layeli Bosco anafafanua kitaalamu kuhusu huduma zinazopatikana, changamoto, na suluhisho.
Ni safari ya sauti, mijadala, burudani, uhalisia wa maisha ya vijana wa Mirerani, na hitaji la kuongeza elimu na huduma rafiki kwa vijana.