Orkonerei FM

‘Mwambie Nimesafiri’: Wajawazito Terrat wapambana na hali zao

28 March 2025, 12:48 pm

Picha kwa msaada wa mtandao

Katika jamii nyingi za Kitanzania, ujauzito ni safari ambayo inapaswa kuwa ya wawili, lakini kwa wanawake wengi wa maeneo ya vijijini kama Terrat, safari hiyo inageuka kuwa ya upweke, huzuni na changamoto kubwa.

Kupitia simulizi ya sauti yenye mguso wa kipekee, inayojulikana kama Mwambie Nimesafiri mtangazaji na mwandishi wa Orkonerei FM Radio Isack Dickson, anachora picha halisi ya namna mila na desturi zimewafanya baadhi ya wanaume kushindwa kushiriki kikamilifu katika huduma za afya ya uzazi kwa wake zao.

Katika sauti hiyo, tunasikia ushuhuda kutoka kwa Magdalena Soipe, mkazi wa Terrat, ambaye anaeleza kwa uchungu jinsi ambavyo wanawake wanahangaika kupata huduma za kliniki bila msaada wa waume zao. Anasema baadhi ya wanaume huona ni aibu kufuatana na wake zao kliniki, wengine wakitumia visingizio vya “kusafiri.