Orkonerei FM

Harambee ya Ujenzi wa nyumba ya Mapadri Engaruka yakuzanya zaidi ya Milioni 13.

29 October 2024, 12:15 am

Mgeni Rasmi wa Harambee, ndugu Daniel Porokwa(mwenye miwani) alipowasili Engaruka.

Zaidi ya Shilingi milion kumi na tatu (13) na mifuko 9 ya saruji zimepatikana katika harambee ya kuchangia ujenzi wa nyumba ya Mapadri Kanisa la Katoliki Kigango cha Engaruka, Parokia ya Mtakatifu Yuda Thadei Mto wa Mbu wilayani Monduli.

Na Baraka David Ole Maika.

Harambee hiyo ya kuchangia ujenzi wa nyumba ya Mapadri katika Kigango cha Engaruka imefanyika siku ya Jumapili tarehe 27.10.2024 katika Kanisa la Katoliki Engaruka imehudhuriwa na watu mbalimbali wakiwepo Viongozi wa Kanisa kutoka Parokia ya Mtakatifu Yuda Thadei, Makatekista, Waumini wa Kanisa la Katoliki na Waumini kutoka makanisa mengine, Waimbaji binafsi wa nyimbo za injili pamoja na Viongozi wa mila.

Baadhi ya Waumini waliohudhuria Harambee ya ujenzi wa nyumba ya Mapadri Kigango cha Engaruka.

Akisoma taarifa ya maendeleo ya mradi wa ujenzi ya nyumba ya Mapadiri Kigango cha Engaruka, mwenyekiti wa kamati ya ujenzi Bw Kastuli Geemay Sukum amesema kuwa ujenzi wa nyumba hiyo ya Mapadri imeanza March 2024 na hadi hapo ilipofikia imefanikishwa na michango ya waumini wa Kanisa la Katoliki Kigango cha Engaruka kupitia sadaka zao pamoja na michango waliojiwekea kila wiki na Jumapili ya kwanza ya mwezi, michango ya Jumuiya na Kanda zinazounda Kigango cha Engaruka.

Sauti ya Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi Bw. Kastuli Geemay Sukum.

Aidha Bw Kastuli Geemay Sukum amesema kuwa hadi sasa ujenzi wa nyumba ya Mapadri Kigango cha Engaruka imefikia hatua ya madiridha na imeshatumia zaidi ya shilingi milioni 7 na ujenzi huo hadi kukamilika utagharimu shilingi milioni 60.

Sauti ya Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi Bw. Kastuli Geemay Sukum.

Mgeni rasmi katika Harambee hiyo ya kuchangia ujenzi wa nyumba ya Mapadri Kigango cha Engaruka Ndugu Daniel Porokwa amesema kuwa hatakata tamaa kushiriki shughuli za maendeleo ndani ya jamii ikiwepo kujenga kanisa hata kama hana pesa kwani wakati wa harambee ukifika pesa zinapatikana.

Sauti ya Mgeni Rasmi ndugu Daniel Porokwa.

Ndugu Porokwa amesema kuwa Kanisa la Katoliki ni kanisa kubwa na lenye nguvu duniani na liko bega kwa bega na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ujenzi wa taasisi za maendeleo ikiwepo Shule, Vyuo na Hospitali.

Sauti ya Mgeni Rasmi ndugu Daniel Porokwa.

Aidha Ndugu Porokwa amewapongeza waumini wa Kanisa la Katoliki Kigango cha Engaruka na Watanzania wote kwa kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ngazi ya Chama na kuwasihi wajitokeze kwa wingi kujiandikisha kwenye Daftari la kudumu la wapigakura pamoja na kushiriki kikamilifu kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 kuwachagua Madiwani, Wabunge na Raisi.

Sauti ya Mgeni Rasmi ndugu Daniel Porokwa.
Mgeni Rasmi wa Harambee ya Ujenzi wa Nyumba ya Mapadri Kigango cha Engaruka Ndg Daniel Porokwa(kulia) akiwa na Viongozi wa Parokia ya Mtakatifu Yuda Thadei Mto wa mbu.

Akitoa neno la shukurani kwa niaba ya Kanisa Kaimu Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Yuda Thadei Father Innocent Abenawe amesema kuwa anawashukuru wote walioshiriki harambee hiyo ya ujenzi wa nyumba ya mapadri kwa kutoa pesa, nguvu na mali zao kufanikisha ujenzi huo

Sauti ya Kaimu Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Yuda Thadei Father Innocent Abenawe.
Waumini wa Kanisa la Katoliki Kigango cha Engaruka.