Orkonerei FM

Ole Sendeka ateta na wananchi, awaondolea hofu

14 August 2024, 12:49 pm

Mbunge Christopher Ole Sendeka

Picha na Evanda Barnaba

Na mwandishi wetu

Mmoja wa wakaazi katika kata ya Terrat wilayani Simanjiro mkoani Manyara alipata nafasi ya kuwasilisha kero ya barabara pamoja na swala la aridhi mbele ya Mbunge wa Simanjiro Chistopher Ole Sendeka katika viwanja vya soko Terrat.

Mweshiwa Mbunge Christopher Ole Sendeka amesema tayari mkataba wa barabara hiyo ilishasainiwa kilichobaki sasa serikali kupitia mikataba hizo na kubainisha gharama

Aidha kwa upande wa pori tengefu mweshimiwa mbunge huyo aliweza kuwatoa wasiwasi wananchi kuwa serikali itaweka utaratibu ya kuhakikisha inalinda maeneo ya malisho ya wafugaji

Kwa upande mwingine Mzee Jumanne mkopi maarufu katika kata ya Terrat aliweza kumkumbusha Mbunge wa Jimbo la Simanjiro Mweshimiwa Ole Sendeka na viongozi wengine kitaifa kukumbuka na kuenzi maeneo ya malisho yanayofahamika kama ranch.

Hayo ni katika ziara ya mbunge huyo pamoja na kamati ya siasa wilaya katika kata ya Terrat viwanja vya soko Terrat.