Orkonerei FM

Makala: Maji safi na salama, athari za ukame Simanjiro

26 July 2024, 4:12 pm

Picha kwa msaada wa mtandao

Na Waandishi wetu

Simanjiro ni moja ya wilaya zinazokumbwa na changamoto kubwa ya ukame, ambayo imeathiri sana upatikanaji wa maji safi kwa wakazi wake. Ukame huu umesababisha vyanzo vingi vya maji kukauka na hivyo kuathiri maisha ya jamii za wafugaji na wakulima. Kulingana na ripoti ya mwaka 2022, zaidi ya mifugo 92,000 ilipoteza maisha kutokana na ukosefu wa maji​

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), maji safi na salama ni yale yanayokidhi viwango vya ubora wa maji kwa matumizi ya binadamu, na yanafaa kwa kunywa, kupika, kuoga, na matumizi mengine ya nyumbani bila kuhatarisha afya.​

Karibu kusikiliza makala hii ya Kurunzi Maalum kutoka Orkonerei FM Radio kupata elimu zaidi kuhusu maji safi na salama na hali ilivyo kwa kata ya Terrat Simanjiro mkoani Manyara.