Orkonerei FM

Namna Umeme unavyochangia maendeleo Kata ya Terrat,Simanjiro

12 July 2024, 11:51 am

picha msaada wa mtandao

Na Isack Dickson.

Kwa mujibu wa REA hadi January 2024, usambazaji wa umeme vijijini umefikia asilimia 80 tangu kuanza kwa utekelezaji wa Mradi wa Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili mwezi Julai 2018 Na, kuna vijiji 758 vilivyobaki kati ya vijiji 12,315 vilivyopo nchi nzima, na wakandarasi wote waliopewa zabuni wamefikia asilimia 75.

Wakala utaanza kufikisha umeme katika vitongoji vyote kulingana na upatikanaji wa fedha baada ya kukamilisha vijiji vilivyofikiwa na huduma ya umeme.

Haya ni mafanikio makubwa na hapa kwenye Makala ya Kurunzi tunaangalia maendeleo yaliyotokana na uwepo wa nishati hiyo. Karibu kuisikiliza.