Orkonerei FM
Migogoro ya ardhi inavyoathiri maendeleo
5 July 2024, 12:02 pm
Kurunzi Maalum
Migogoro ya ardhi ni hali ya kutokubaliana au mvutano kati ya pande mbili au zaidi kuhusu umiliki, matumizi, au mipaka ya ardhi.
Migogoro hii inaweza kusababishwa na sababu mbalimbali kama vile upanuzi wa shughuli za kilimo na ufugaji, uwekezaji katika ardhi, ukosefu wa hati miliki za ardhi, mabadiliko ya tabianchi, na mipango duni ya matumizi ya ardhi.
Katika makala hii maalum ya Kurunzi ambayo hukujia kila Ijumaa saa 2:30 asubuhi kupitia ORKONEREI FM wiki hii imeangazia namna Migogoro ya ardhi inavyokwamisha maendeleo kwenye jamii, hapa utasikia visa lakini ufafanuzi wa namna gani migogoro imekwamisha maendeleo.
Karibu kuisikiliza makala hii maalum.