Ongezeko la mifugo linavyotishia uhai wa ushoroba wa Kwakuchinja
8 May 2024, 10:46 am
Na Isack Dickson.
Tanzania ikiwa moja ya nchi zenye mkakati wa kuongoa shoroba bado, inaendelea na jitihada hizo kuhakikisha mapitio ya wanyama yanakua salama.
Kwa mujibu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Tanzania ina jumla ya shoroba 61 ambapo 41 ikiwemo ya Kwakuchinja, zipo hatarini kutoweka kutokana na kuvamiwa na shughuli za kibinadamu huku shoroba 20 kati ya hizo zikiwa zimezibwa kabisa.
Ongezeko la mifugo kwenye vijiji vilivyopo pembezoni mwa ushoroba wa Kwakuchinja vinarudisha nyuma jitihada za Serikali ya Tanzania kuweka salama ushoroba huu.
Ili kufahamu mengi zaidi fuatana na mwanahabari Isack Dickson aliyefunga safari na kuweka kambi katika kijiji cha vilima vitatu kufuatilia namna ongezeko la mifugo linavyotishia uhai wa Ushoroba wa kwakuchinja,karibu kuisikiliza makala hii.
https://radiotadio.co.tz/orkonereifm/wp-content/uploads/sites/37/2024/05/makala-kamili.mp3