Karagwe FM

Recent posts

6 July 2023, 8:51 pm

Wananchi Karagwe wamshukuru Rais Dkt. Samia kwa miradi ya maendeleo

Baadhi ya wananchi wa wilaya ya Karagwe mkoani Kagera wameishukuru serikali kwa kutekeleza miradi ya maendeleo katika maeneo yao. Na Ospicia Ddace Wananchi wa wilaya Karagwe wameishukuru na kuipongeza serikali ya Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa miradi mikubwa…

4 July 2023, 1:04 pm

28 wapigwa msasa kwa ajili ya Uokoaji

Jumla ya Askari 28 wa Jeshi la zimamoto na Uokoaji kutoka mikoa mbalimbali Nchini Tanzania wameshiriki mafunzo ya pamoja ili kujiongezea ujuzi utakaowasaidia wakati wa uokoaji yanapotokea majanga. Akifungua mafunzo hayo Nov 21 mwaka huu,Kamishina msaidizi mwandamizi Zabrune Levson Muhumha,Kamanda…

4 July 2023, 11:38 am

Jela miaka 30 kwa ubakaji wa mtoto

Mahakama ya wilaya ya Missenyi mkoani Kagera, imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela Mahmoud Idi (54) mkulima mkazi wa kijiji cha Kigarama kata ya Kanyigo wilayani humo kwa kuthibitika pasipo na shaka kuwa alimbaka mtoto wa miaka minane kijijini hapo…

4 July 2023, 11:18 am

Karagwe: DC aridhishwa utekelezaji wa miradi ya elimu

Mkuu wa wilaya ya Karagwe Julius Laiser akiwa katika shule ya msingi Kambarage iliyopata fedha za mradi wa boost: Picha na Eliud Henry Mkuu wa wilaya ya Karagwe Julius Laiser amekagua na kuridhishwa na ujenzi wa vyumba vya madarasa chini…

3 July 2023, 12:44 pm

Karagwe: Wanaodaiwa kununua ardhi kinyemela watakiwa kuwasilisha nyaraka kwa DC

Serikali wilayani Karagwe imetoa siku saba kwa wananchi walionunua ardhi ya kijiji cha Kahanga kata ya Nyakasimbi wilayani humo  kinyume cha sheria kuwasilisha vielelezo vitakavyowezesha kubaini wahusika waliowauzia  ardhi hiyo. Na Eliud Henry Wakizungumuza katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na…

2 June 2023, 10:32 pm

Katibu CCM Karagwe: Leeni watoto kimaadili

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya Karagwe Bw. Anathory Nshange amewataka wazazi na walezi kulea watoto wao katika maadili ya kitanzania na kiimani Bw. Nshange ameyasema hayo wakati akiongea kwenye mahafali ya tano ya chuo cha Karaduce wilayani Karagwe…

2 June 2023, 10:17 pm

Homa ya marburg Kagera yatokomezwa

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ameutangazia ulimwengu kuwa Kagera na Tanzania ni salama dhidi ya ugonjwa wa marburg na kwamba hakuna tena ugonjwa huo. Pamoja na hayo waziri Ummy pia amewashukuru watumishi wa wizara ya afya pamoja na mashirika ya…

KARAGWE FM PROFILE

UTANGULIZI.
Radio Karagwe ni Radio ya kijamii iliyoanzishwa na shirika lisilokuwa la kiserikali lijulikanalo kama Karagwe Media Association (KAMEA).Ilianza kurusha matangazo yake Desemba 11.2007 kupitia masafa ya 91.4 MHz kwa ufadhili wa shirika la nchini Denmark (ULD80 Karagwe Venor) waliowezesha mafunzo kwa watumishi na upatikanaji wa vifaa.

DIRA.
Kuziba pengo la mawasiliano kwa wananchi wa Karagwe ambao kwa wakati huo hawakuwa na uwezo wa kusikiliza radio za Tanzania kutokana na jiongrafia ya eneo.

MAENEO REDIO INAKOSIKIKA
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na ULD80 June mwaka 2012 Radio Karagwe ina zaidi ya wasikilizaji milioni 1.2.(KM 200 KUTOKA MAKAO MAKUU).Inasikika katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Kagera,katika wilaya za Karagwe, Kyerwa, Missenyi, Muleba na Bukoba Vijijini. Inasikika katika maeneo machache wilaya za Ngara, Biharamulo na Bukoba manispaa. Pia inasikika maeneo ya nchi jirani za Uganda, Burundi na Rwanda.

MAWASILIANO.
S.L.P 316,KARAGWE KAGERA TZ
E-mail : radiokaragwe@gmail.com
Phone: +255 754 677 708 / +255 689 471 171