Sengerema FM

TARI-Ukiligulu waja na mbegu bora kukabiliana na magonjwa ya zao la mhogo.

16 October 2021, 1:26 pm

Kitalu cha kuoteshea mbegu mpya za zao la mhongo kilichopo katika tasisi ya utafiti TARI -Ukiliguli Misungwi Mwanza

Katika kupambana na magonjwa yanayolikabili zao la mhogo, Wakulima wa zao hilo kanda ya ziwa wameshauriwa kutumia mbegu bora inayozalishwa na taasisi ya utafiti TARI -UKILIGULU MWANZA, ambayo inastahimili magonjwa.

Akizungumza na waandishi wa Habari Mtafiti upande wa mazao ya mizizi Bwn.Kasele Salum amesema wamekuwa wakizalisha mbegu bora ya mhogo inayostahimili magonjwa kwa Kanda ya ziwa,ambapo huwauzia wakulima wazalishaji kwa lengo la kwenda kuwauzia wakulima watumiaji.

Aidha Bwn. Salum amewashauri wakulima wa zao la mhogo kuachana na mfumo wa kusambaziana mbegu kienyeji kwani hali hiyo imekuwa isababisha kusambaa kwa magonjwa ya mhogo nakwamba wakulima wanashauriwa kuvuna kuanzia miezi kumi na isizidi miezi kumi na mbili ili kuepusha mhogo kuathiliwa na magonjwa.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa TARI-UKILIGULU MWANZA Dkt. Heneriko Kulembeka amesema kituo hicho kinaratibu mazao ya mizizi nchi Tanzania.

Hata hivyo zao la mhogo ni zao tegemezi kwa chakula katika kanda ya ziwa lakini zao hilo limekuwa likikabiliwa na changamoto ya magonjwa hususani kwa wakaazi wa Wilaya ya Sengerema ambayo kwa mjibu wa sensa ya watu na makazi yamwaka 2012, inakadiliwa kuwa na Zaidi ya watu laki 6 ambao ni wakulima na hujishugulisha na kilimo cha mhogo kwa ajili ya chakula.

Ni Mwandishi wetu Michael Mgozi akiripoti Taarifa ya zao la mihogo kutoka Ukiligulu Misungwi