Sengerema FM

Makamu wa rais atoa maagizo mazito kwa TRA Nchin

4 April 2021, 8:54 pm

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Philipo Mpango akitoa salamu za pasaka leo jijini Dodoma.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango amewataka Watumishi wote wa Umma na Watanzania kufanya kazi kwa Bidii, Uadilifu na weledi pamoja na  kumtanguliza Mwenyezi Mungu.

Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Mpango ameyasema hayo leo April 04,2021 katika Ibada ya Misa Takatifu ya kuadhimisha Sikukuu ya Pasaka iliyofanyika katika Kanisa Kuu Katoliki Jimbo Kuu la Dodoma.

Aidha Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango ameitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA kukusanya kodi kwa kuzingatia sheria za Nchi na kuwaacha Wafanya Biashara wafanye Biashara zao kwa  Haki na kutowanyanyasa kwenye Biashara zao ili kuleta kodi kwa ajili ya kuweza kuwahudumia Watanzania.

Katika Ibada hiyo Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Mpango pia amewasilisha salam za Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuwaomba Waumini hao na Watanzania kwa ujumla waendelee kumuombea Rais Samia na kuiombea Nchi ili iweze kuneemeka zaidi  ya hapa ambapo Rais Hayati Dkt. John Pombe Magufuli ametufikisha.

Zaidi msikirize hapa ………….