Pambazuko FM Radio

Chanjo ya kichaa cha Mbwa

22 February 2023, 3:31 pm

Isidory Matandula

 Imeelezwa kuwa asilimia 99 ya watu wanaokufa kutokana na ugonjwa wa kichaa cha mbwa, wanakufa kwasababu waling’atwa na Mbwa mwenye kichaa na asilimia moja tu ndio wanakufa kwa kung’atwa wanyama wengine .

sauti ya dkt. maganga

Hayo yamebainishwa na Dkt Sambo Maganga wa Taasisi ya  Afya Ifakara (IHI), Februari 18, mwaka huu, mjini Ifakara, katika mkutano wa viongozi wa jamii na wadau wa afya, kutoka maeneo yanayofanyiwa utafiti wilayani Malinyi mkoa wa Morogoro.

Dkt. Maganga akijibu maswali ya wajumbe wa mkutano
wajumbe katika mkutno wa kutathmini miradi ya utafiti – idara ya EHES bonde la Kilombero

Dkt. Maganga amebainisha kuwa Mbwa huchanjwa kwa gharama kati ya  shilingi 1,500 hadi shilingi elfu tano, na kwa upande wa binadamu amesema chanjo yake inapatikana kati ya  shilingi elfu 30,000 hadi elfu 35,000 kwa dose moja, ambapo mtu mmoja anatakiwa kupata dozi moja hadi tatu ili kujikinga na kichaa cha Mbwa.

Utambuzi wa  kiasi cha maambukizi ya kichaa cha mbwa na kutoa chanjo ni moja ya miradi mitano mipya inayotekelezwa na Idara ya EHES kwa sasa inayozingatia ikolojia na maambukizi ya magonjwa ya kuambukiza .

Sauti ya fadhili matandiko akiuliza swali kuhusu chanjo ya mbwa
sauti ya Dkt Maganga akielezea gharama za chanjo ya mbwa
sauti ya dkt maganga akijibu swali kuhusu chanjo ya mtu aliyeng’atwa na mbwa