Orkonerei FM
Orkonerei FM
22 December 2025, 9:30 am

Na Isack Dickson,
Katika Wilaya ya Simanjiro, mabadiliko ya tabianchi si hadithi tena, bali ni ukweli mchungu unaohatarisha usalama wa chakula, hata hivyo kundi la wanawake 111 katika vijiji 5 limeamua kubadili mwelekeo. Kupitia ushirikiano na shirika la TACCEI, wanawake hawa wamegeuza ardhi kame kuwa mashamba ya kijani kibichi kwa kutumia teknolojia rahisi ya umwagiliaji.

Makala hii ya kusisimua inakupeleka Simanjiro kusikia simulizi ya Vaileth Kadogo na wenzake, ambao si tu wanatunza mazingira, bali wanatekeleza kwa vitendo malengo ya Agenda 2063 ya Afrika na SDG 5 kuhusu usawa wa kijinsia.
