Orkonerei FM
Orkonerei FM
28 November 2025, 6:11 pm

Baadhi ya wanawake wakiwa katika mafunzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Manyara Hall -Ilaramatak Terrat Simanjiro kuhusu kuendana na adhari za mabadiliko ya tabianchi yaliyotolewa na shirika lisilo la kiserikali la PINGOs Forum leo Novembar 28,2025 (picha Evanda Barnaba).
Na Joyce Elius
Shirika la pingo,s foram leo limeendesha mafunzo maalumu kuhusu mabadiliko ya tabia nchi yakilenga kuongeza uelewa na uwezo wa jamii kukabiliana na athari ya zake.
Akizungumza na Orkonerei fm Meneja msaidizi Hopejoanne Wandera wa shirika hilo amesema lengo la mafunzo hayo ni kutoa mrejesho wa mafunzo yaliyofanyika kipindi cha kwanza na kuhusu mabadiliko ya tabia ya nchi na athari zake hasa kwa wafungaji.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wameleza kufurahishwa na mafunzo hayo waliyoipata wakasema imewasaidia kuelewa kwa kina namna mabadiliko ya tabia nchi yanavyoathari masisha yao ya kila siku.
Wananchi hao wameeleza matarajio yao baada ya kupokea mafunzo hayo wakisema watumia elimu waliyoipata itakuwa chachu ya mabadiliko chanya katika jamii.