Orkonerei FM
Orkonerei FM
28 November 2025, 9:14 am

KURUNZI MAALUMU
Katika hali ya ukame uliokolea na utegemezi wa mvua, hasa Manyara, Orkonerei FM inakuletea Kurunzi Maalumu inayoangazia Kilimo cha Umwagiliaji kama mkombozi mkuu. Sikiliza jinsi wakulima wa Kata ya Terrat, Simanjiro, wanavyotumia vyanzo vidogo vya maji kama korongo kufanya kilimo cha mboga mboga na mazao mengine mwaka mzima, wakijiongezea kipato na kuhakikisha familia zinapata chakula.
Kipindi hiki kinakuletea sauti za wakulima wadogo na wakubwa waliofanikiwa, Aliyekuwa Afisa Kilimo wa Kata anayeeleza umuhimu wa umwagiliaji kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, na Diwani wa Terrat Jackson Matery akizungumzia mikakati ya miundombinu. Ni mwongozo kamili wa jinsi ya kugeuza changamoto ya ukame kuwa fursa ya mafanikio ya kiuchumi!