Orkonerei FM

Ukatili wa kijinsia bado ni changamoto

25 November 2025, 1:19 pm

Picha kwa msaada wa mtandao

Kuelekea maadhimisho ya Siku ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia Duniani, wananchi wameendelea kukumbushwa umuhimu wa kulinda haki, usalama na utu wa wanawake, wanaume na watoto katika jamii

Akizungumza Orkonerei fm kupita kipindi cha mchaka mchaka kwa njia ya simu Bi Nambaya Haji Afisa Ustawi wa Jamii,wa mji Mdogo wa Mererani amesema kuwa baadhi ya wazazi bado wanawaacha watoto wao bila uangalizi jambo linalosababisha watoto kujilea wenyewe.

Ameongeza kuwa wazazi wengi wanatoa sababu mabilimbali kama majukumu ya kutafuta riziki lakini amesisitiza kuwa kutafuta maisha hakupaswi kuwa sababu ya kuacha watoto bila uangalizi.

Pia ametoa wito kwa malagwanani, viongozi wa mitaa na wadau wa jamii kuongeza juhudi za kutoa elimu kwa jamii na kuachana na mila potovu hasa ukeketaji.